Kukosa choo kwa siku moja
kitaalamu, siyo tatizo, isipokuwa mtu anaweza kutajwa kuwa na tatizo hilo
iwapo atakosa choo kwa angalau zaidi ya saa 72, yaani siku tatu.
kawaida kila mtu anatakiwa
apate choo angalau mara tatu kwa wiki. “Kama mtu atakosa choo kwa siku tatu
mfululizo, atahesabika kuwa na tatizo, lakini lazima awe amekula chakula kwa
siku zote hizo.
Mtu ambaye hajala hawezi kuhesabika kuwa na
ugonjwa huo bali atakuwa na tatizo jingine.
Zipo sababu nyingi
zinazosababisha tatizo la haja kubwa zikiwemo za kutojizoeza kwenda haja kubwa
mara kwa mara, kula vyakula vilivyokobolewa, matumizi mabaya ya dawa,
mabadiliko ya homoni na magonjwa mengine ya mwili,kuwa na msongo wa mawazo pia kunaweza kupelekea mtu kutokupa choo.
MATATIZO YANAYOSABABISHWA NA KUKOSA CHOO.
Kukosa choo linaweza kuwa
tatizo, lakini kama halitapatiwa ufumbuzi linaweza kuzaa matatizo mengine
mwilini.
Dalili za kuwa na
tatizo la kukosa ni kwamba mgonjwa anaweza kupata maumivu ya tumbo ambayo
hutokana na tumbo kujaa gesi. Mtu mwenye tatizo la kukosa choo mara nyingi
tumbo lake huvimba na kujaa gesi muda wote, hali hii inatokana na kuwa na
uchafu tumboni.
Pia kukosa choo kunaweza pia
kusababisha maambukizi katika utumbo ambayo yanaweza pia kusababisha magonjwa
mengine ukiwamo wa kuoza kwa sehemu ya utumbo.
Kinyesi kinapokwama mahali,
eneo lile linaweza kukandamizwa na kukosa damu, hivyo linaweza kuoza.
Ugonjwa mwingine unaoweza
kuupata kwa kukosa choo ni uvimbe katika njia ya haja kubwa
(Bawasiri) ambao nao husababishwa na kuchubuka mara kwa mara wakati wa
kujisaidia.
Ngozi ya njia ya haja kubwa
inapopata michubuko mara kwa mara, hupasuka na kusababisha vivimbe vidogo
ambavyo huweza kukua kadri hali hiyo inayoendelea.
WAKINA NANI HUUGUA HUU UGONJWA.
Kwa kawaida tatizo hili huwapa
watu mbalimbali duniani kote, lakini hutofautiana ukubwa wake kutokana na mifumo ya maisha, kwani wengine huwa wepesi kuligundua na kulitafutia ufumbuzi.
Karibu kila mtu duniani katika hatua fulani ya maisha hupata tatizo hili,
kutokana na sababu za vyanzo vyake watu hupitiwa au kwa makusudi huacha kufuata
kanuni na kujikuta wamepata tatizo hili.
Mfano wakati wa
sherehe au mikusanyiko ya watu huwa ni vigumu kuchagua aina ya vyakula na
wakati mwingine matunda na maji ya kutosha hukosekana hivyo kuwafanya watu wale
vyakula vigumu ambavyo vinaweza kuchochea tatizo hili.
Dawa ya kutibu tatizo la kukosa choo |
Kinga na matibabu yake
Kila mtu anao uwezo wa
kujikinga na tatizo hili kwa kufuata kanuni za ulaji chakula bora.
Njia sahihi ya kujikinga na
ugonjwa huo ni kula nafaka zisizokobolewa, matunda, mboga mboga na kunywa maji
kwa wingi.
Kuhusu matibabu halisi iwapo
tatizo litagundulika mapema ni rahisi kulikabili kwa kubadilisha mfumo wa ulaji
akitolea mfano mtu anapokosa choo na kuamua kula mapapai kwa wingi .
Kama mgonjwa akishindwa
kutumia tiba mbadala ambazo ni pamoja na kula matunda, mboga na kunywa maji
mengi, anaweza kutibiwa kwa kupewa dawa mbalimbali kama ALOE ambazo zinaweza kumsaidia
ili apate choo.
Hata hivyo, hilo
linaposhindikana kwa njia zote hizo, mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji mdogo
ili kuondoa kinyesi kile kilichoganda na kumwanzishia matibabu ya kumfanya
aweze anajisaidia kwa urahisi.
wasiliana nami kujipatia dawa kabla tatizo halijawa kubwa.
+255 787 218159
+255 764 218159
0 comments:
Post a Comment