Insomnia ni nini?
Huu ni ugonjwa ni ugonjwa ambao huambatana na tabia
zifuatazo..
- Kushindwa kupata usingizi kabisa.
- Kulala na usingizi kuisha usiku sana na kushindwa kulala tena.
- Kubadilika kwa mfumo wa kulala mfano mtu wa aina hii husinzia mchana na kukosa usingizi usiku.
- Kusinzia haraka baada ya kufika kitandani na usingizi kuisha haraka kisha kushindwa kupata usingizi tena.
Ugonjwa huu husababishwa na nini?
- Utumiaji wa madawa kama cocaine, nicotine,cafaine na unywaji wa pombe uliopitiliza.
- Magonjwa ya moyo ambayo humfanya mtu ashindwe kupumua vizuri wakati wa kulala.
- Maumivu makali ya mwili kama kidonda, kuvunjika mfupa, misuli na kadhalika.
- Matatizo ya mfumo wa chakula kama kiungulia na kupata choo ngumu.
- Mazingira mabaya ya kulala kama kelele nyingi na harufu kali.
- Msongo mzito wa mawazo
- Magonjwa ya akili mfano schizophrenia na dementia.
- Utumiaji wa ovyo wa dawa za kuleta usingizi mfano diazepam maarufu kama valiam.
- Upungufu au ongezeko la homoni za uzazi hasa kipindi cha uzeeni kwa wanawake{menopause} .
MATIBABU
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyka katika sehemu kuu mbili
kama ifuatavyo.
Matibabu yasiyotumia dawa{non pharmacological treatment}:
kikubwa kinachofanyika hapa ni kuacha tabia zote ambazo ziko
ndani ya uwezo wako ambazo zinakufanya ukose usingizi kama nilivyozianisha hapo
juu. Aina hii ya matibabu ni nzuri na bora zaidi kuliko matumizi ya dawa za
kuleta usingizi ambazo mara nyingi zinasababisha kuzitegemea yaani bila hizo
haulali{dependence} na kuleta madhara mengine ya kiafya.
- Usile chakula kingi wakati wa kwenda kulala.
- Usinywe kahawa wakati wa kwenda kulala
- Kitanda kitumike kama sehemu ya kulala sio kuangalizia video na kucheza game.
- Usiangalie video za kutisha wakati wa kwenda kulala.
Matibabu ya dawa
Magonjwa yanayosababisha{underlying causes} mtu kushindwa kulala
yanatakiwa yatibiwe kwanza. mfano maumivu
makali ya mwili kutokana na magonjwa
flani.
dawa ya kutibu tatizo la kutopata usingizi ni MELATONIN SOFTGEL CAPSULES
kuipata dawa wasiliana nami kwa simu no +255787218159
0 comments:
Post a Comment