Habari mpendwa msomaji wa makala zangu za kilimo na afya natumaini u buheri wa afya na unaendelea na shughuli zako kama kawaida.
Leo tutaenda kujifunza aina za mbolea na matumizi yake hasa mbolea zile ambazo ni mbolea asilia ambazo hazina madhara katika mazao,ardhi na kwa binadamu pia.
🌴Kuna aina mbali mbali za mbolea kama mkulima umewahi kukutana nazo au umewahi kuzitumia kwa namna moja au nyingine,tuna aina kuu mbili za mbolea yani mbolea ya asili(organic fertiliser) kama vile BIO PLUS, SAMADI,MBOJI nk na ile ya viwandani iliyochanganywa na kemikali(inorganic fertiliser) kama vile MIJINGU,UREA,NPK,TSP,DAP na nyingine nyingi unazozifahamu.
🌴Kwa miaka ya hivi karibuni mbolea za viwandani zimeshika kasi katika matumizi ya kilimo huku zikituachia madhara katika mazao, ardhi na hata kwa binadamu pia hivyo inabidu turejee katika matumizi yetu ya mbolea ya asili ambayo imetumika enzi na enzi za mababu zetu na wakawa wanajitosheleza kwa chakula na huku ardhi zao zikiendelea kuwa na rutuba.
🌴Ikumbukwe tu kwamba mimea inaweza kumea sehemu yoyote ile kama mazingira mmea ulipo unavirutubisho vya kutosha kuufanya huo mmea kukua na kusitawi vizuri.sio tu lazima mimea imee kwenye udongo hvyo mbolea pia ni kirutubisho moja wapo kinachopolekea mmea kuota na kukua.
🌴Mbali nakuwa na mbolea za viwandani na za asili pia kuna mbolea za kupandia mazao na za kukuzia vilevile ikumbukwe kuwa kuna mbolea ambazo zinaweza kufanya hizo kazi zote yani kupandia na kukuzia mazao.
FAIDA ZA KUTUMIA MBOLEA ZA ASILI KATIKA KILIMO.
🌴 Ni rafiki kwa mazingira mbolea zote za asili hazi madhara katika mazingira.
🌴Mbolea za asili zinarutibisha ardhi kwani huwa na mazingira mazuri yanayopeleka bacteria kuzaliana na kuoza na hivyo kupelekea ardhi kuwa na rutuba wakati wote utakao tumia mbolea ya asili katika shamba lako.
🌴Inasaidia kukuza mizizi na kuipa uwezo wa kufyonza madini muhimu yanayohitajika katika mimea.
🌴Inausaidia mmea kutengeneza kijani kibichi ambacho mmea hujitengenezea chakula kutokana na hicho kijani kibichi.
🌴Ni rahisi kuitumia,kupatikana na utengenezaji wake pia ni rahisi.
Kuna faida nyingi sana utakazozipata endapo utatumia mbole ya asili katika kilimo chako.
Makala hii inashia hapa kwa leo tukutane siku nyingine katika mwendelezo wake ambapo tutajifunza namna gani ya kuandaa shamba,kutumia mbolea za asili kwa kila zao na vipimo vyake.
Kama una swali maoni usisite kuniandikia kupitia kisanduku cha maoni hapo chini👇👇👇👇au tuma ujumbe whatsapp kupitia simu no 0787218159.
0 comments:
Post a Comment