Vidonda vya tumbo ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi, wanaume na wanawake na hata watoto wadogo. Tatizo hili husumbua sana na kumfanya mgonjwa asiweze kumudu shughuli zake za kila siku.
Ugonjwa huu huathiri kwa ujumla katika suala zima la afya.
Tatizo hili huanza taratibu na dalili za awali huwa hazionyeshi kama mtu ana ugonjwa huu.
Chanzo cha ugonjwa
Ugonjwa huu hutokana zaidi na maambukizi ya bakteria waitwao ‘Herictobacter Pylori’ au maarufu kama H. Pylori hushambulia tabaka la ndani la tumbo.
Aina hii ya bakteria ni wagumu kufa kwa kuwa wana uwezo wa kuishi kwenye mazingira ya tindikali tumboni. Tumboni kuna tindikali ya Hydrochloric Acid ambayo husaidia katika mmeng’enyo wa chakula.
Bakteria hawa wanaposhambulia tabaka la ndani la kizazi, hutegemea vishimo vishimo ambavyo ni vidonda hivyo tindikali inapotoka huchoma kwenye hivyo vidonda na kumfanya mgonjwa ahisi maumivu makali.
Aina za vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo vipo vya aina mbili, kwanza ni vile vilivyopo mwanzoni mwa tumbo la chakula, Gastric Ulcers na ya pili ni Duodenal Ulcers katika sehemu ya pili ya tumbo. Maumivu na dalili za aina hizi mbili hufanana sana.
Ili kutofautisha aina hizi za vidonda, vipimo maalum hufanyika kama vile ‘OGD” na “Barium Meal’, vipimo ambavyo hufanyika katika hospitali za rufaa.
Dalili za ugonjwa
Hapa tutazungumzia dalili kuu za vidonda vya tumbo kwa ujumla. Mgonjwa wa vidonda vya tumbo katika hatua za awali huwa hajigundui kama ana tatizo.
Mgonjwa hulalamika kuhisi homa za mara kwa mara na kujihisi kama ana malaria au homa ya tumbo ‘Taifoidi’, wengine hulalamika kutumia sana dawa za taifoidi lakini hakuna nafuu.
Mwili unanyong’onyea, maumivu ya viungo, kuhisi baridi kuumwa kichwa na tumbo kujaa gesi.
Mgonjwa pia hulalamika maumivu ya tumbo eneo la chembe ya moyo ambapo ni chini ya kifua na juu ya kitovu.
Maumivu ya muda mrefu husambaa tumbo lote na tumbo huunguruma mara kwa mara .
Maumivu ya chembe ya moyo yaani chini ya kifua na juu ya kitovu husambaa hadi kifuani na kuzunguka mpaka mgongoni.
Mgonjwa hulalamika kuhisi moto kifuani na maumivu yaani kiungulia. Akilala usiku hali ya moto huongezeka na mgonjwa akicheua hutoa majimaji ya moto na machungu.
Mgonjwa hupata choo kigumu na vipande vipande kama cha mbuzi na wakati mwingine huwa cheusi.
Mgonjwa hupoteza hamu ya kula na wakati mwingine hutapika damu. Macho hupoteza nguvu ya kuona kwa kuwa muda wote anakuwa na maumivu, mwili unachoka na anakosa raha kutokana na kuwaza sana juu ya maumivu anayopata kiasi cha kumfanya mgonjwa akonde.
Mkojo unakuwa wa njano sana, hufunga kupata choo kikubwa na kusababisha maumivu ya kiuno kwa ndani ambayo husambaa hadi miguuni. Hamu ya tendo la ndoa pia hupotea.
TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO
vidonda vya tumbo vinatibika kwa dawa zilizotengenezwa kwa mboga mboga na matunda na tiba yake huchukua muda mrefu kuanzia mwezi mmoja hadi miezi mitatu kwa mtu kupona kabisa,hivyo kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni muhimu kuzingatia masharti ya dawa anazopewa,
jipatie dawa ya aloe iliyotengenezwa kwa alovera na ganodema iliyotengenezwa kwa uyoga mwekundu kutibu tatizo la vidonda vya tumbo.
wasiliana na mimi kwa maswali na tiba ya vidonda vya tumbo
+255 787 218 159
+255 764 218 159
Tithi's titanium ring for men - Titanium Arts
ReplyDeletetithi's titanium ring for men - Tithi's titanium drill bits titanium ring for titanium blade men. A titanium ring for men - Tithi's titanium nose rings titanium ring for titanium engagement rings for her men. A titanium ring for titanium pickaxe terraria men.