Saturday, 11 July 2015




siku za hivi karibuni, wanawake nchini wamekuwa wakilalamika na wengi wao kukutwa na uvimbe katika nyumba ya uzazi uvimbe huo, ambao si saratani, umekuwa ni tishio kwa maelfu ya wanawake nchini jambo linalosababisha wengi wao kufanyiwa upasuaji na wengine hata kuondolewa vizazi.

Wanapatholojia wanaulezea ugonjwa huu kuwa ni fibroids kwa kitaalamu ‘leimyoma’ ni uvimbe unaowapata asilimia 25 ya wanawake wa Kiafrika na asilimia 50 ya Wazungu.
Uvimbe huu si saratani, unajitokeza ama katika ukuta wa kati, wa nje au ndani kabisa ya nyumba ya uzazi,”
Pia uvimbe huu huwa katika umbile la misuli myembamba na laini na hukua siku hadi siku,sababu kuu ya ugonjwa huu, bado haijajulikana. pamoja na kuwa sababu kuu haijajulikana, lakini zipo sababu ambazo zimehakikiwa kusababisha mwanamke kupata uvimbe wa fibroids.Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya ‘estrogen’ ambavyo vipo katika miili ya wanawake,vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi. “Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu, huwa ni wanawake walio katika balehe au ambao tayari wamevunja ungo, kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogen,Lakini, pia endapo inatokea mwanamke akapata matibabu ambayo yatamtaka kuongezewe vichocheo hivi, huwa katika hatari ya kupata uvimbe huu. ndiyo maana wanawake walio katika kikomo cha hedhi(menopause) na watoto hawawezi kupata uvimbe huu. 

Sifa kuu za ugonjwa huu , huwa ni nyingi kwa sababu ni uvimbe ambao asili yake ni mishipa midogo midogo na inapokuwa huweza kufikia urefu wa sentimeta tano na zaidi na uzito wa kilogram 10.Uvimbe huu unaweza kutokea katika kuta zote za kizazi cha mwanamke na kusababisha mwanamke ang’olewe kizazi chake. “Hata hivyo, wanawake wengi hupata uvimbe huu katika ukuta wa ndani kabisa wa kizazi,
Sifa nyingine za uvimbe huu ni kuwa na tabia yake ya kubadilikabadilika sana.Kwa mfano, fibroids huweza kubadilika rangi na kuwa ya njano, ikabadilika na kuwa katika hali ya kimiminika, baadaye kuwa ngumu au kuwa laini yenye kutomasika.

             Dalili za Fibroids
Ni vigumu mwanamke kubaini au kuhisi dalili zake.“Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa, wengi hugundulika wakati wa kujifungua, na ujauzito au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi, basi huweza kutokwa damu kwa wingi,Hata hivyo, asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,.

Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi. Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo sana zikiambatana na maumivu makali. Asilimia 30 ya wanawake wanaopata maumivu na damu nyingi wakati wa hedhi huwa na uvimbe wa aina hii.Wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe.
Nina mifano hai, wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito, wakakosa kabisa siku zao za hedhi, wakapata dalili zote za ujauzito na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids,mara nyingi uvimbe unaojitokeza katika ukuta wa nje wa kizazi na kuning’nia, ndiyo hucheza na kuleta dalili za ujauzito.Mwanamke huweza kuvimba miguu kwa sababu uvimbe huu husababisha damu isitembee.

Dalili nyingine kuwa ni mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.Wakati mwingine, fibroids hukua na kuzuia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kusababisha mwanamke avimbiwe. Vile vile, uvimbe huo huweza kuzuia kibofu cha mkojo, na kumfanya mwanamke apate haja ndogo kwa taabu , au akatokwa na uchafu ukeni.
Hatari kuu ya uvimbe huu ni ugumba, asilimia 27 hadi 40 ya wanawake wanaopata uvimbe katika kuta zote za kizazi, hushindwa kupata watoto.

Hatari nyingine ni kwa wanawake wajawazito wenye uvimbe huu ambao wengi hufanyiwa upasuaji kwani fibroids huweza kuzuia mlango wa kizazi na mwanamke kushindwa kujifungua. Imebainishwa kuwa, asilimia 30 ya wanawake hutolewa vizazi mara baada ya kujifungua kutokana na uvimbe huu.
Tahadhari, wanawake walio katika umri wa kuzaa lakini hawazai wapo katika hatari ya kupata maradhi haya. Hii ni kwa sababu vichocheo vya estrogen hukua kwa wingi na kusababisha misuli ya fibroids kukua, lakini vichocheo hivyo huacha kukua wakati wa ujauzito.

Walio katika hatari hii ni watawa ambao hawatakiwi kuzaa au wale wanaopitiliza umri wa kuzaa.
Watalaamu mbalimbali wa afya ya uzazi wanashauri wanawake kwenda kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara ili kubaini maradhi ambayo mengine yanaweza kutibika au kuzuilika.

UNGANA NAMI KATIKA SEHEMU YA PILI YA MAKALA HII ITAKAYOKUWA IKIJIBU SWALI LAKO JE NIKWELI UVIMBE KATIKA KIZAZI HAUPONI KWA DAWA TU LAZIMA MGONJWA AFANYIWE UPASUAJI? NA TIBA YAKE.

WASILIANA NAMI
 +255 787 218159
 +255 764 218159

Monday, 6 July 2015

Image result for soya beans
Maharage ya soya




 
 
kirutubisho kilichotengenezwa kwa maharage ya soya



Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kuumia wakati mnafanya tendo la ndoa kwa mwanamke hujulikana kama Dyspareunia.
Utafiti unaonesha kwamba kati ya wanawake watatu, wawili wamewahi au hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Imefikia kwamba baadhi ya ndoa, mwanamke anapata maumivu kiasi cha kutokuwa na hamu tena ya tendo la ndoa na matokeo yake wamekuwa na wakati mgumu linapokuja suala la kufanya mapenzi na pia kila wakirudia kufanya tendo la ndoa, mambo yamekuwa ni yaleyale kwa mwanamke kuumia zaidi kuliko mara ya kwanza.
Kawaida huwa haifurahishi kabisa na haina hata ladha kufanya tendo la ndoa huku mmoja kati yenu akiwa anapata maumivu makali au shida hiyo husababisha kutojishughulisha katika kuleta raha ya kweli na hatimaye kuridhishana kimapenzi wakati wa tendo la ndoa.
Tendo la ndoa halikuwekwa ili kukupa shida au maumivu bali kukupa raha, furaha na kuridhishwa.
Moja ya kanuni muhimu sana katika tendo la ndoa ni “ Kama unapata maumivu usifanye”
Badala yake tafuta nini kimesababisha na tafuta jibu sahihi la kuondoa hiyo hali au muone daktari akusaidie.

Na baada ya kupata tiba na kupona ndiyo unaruhusiwa kuendelea kufanya tendo la ndoa kwa kufurahia na kukupa raha zaidi, vinginevyo itakuwa ni kuleta maangamizi.
Ni kweli kwamba kama moja wapo ya mahitaji ya msingi ya kihisia (emotions) kama hili tendo la ndoa halipatikani katika ndoa linaweza kusababisha mmoja ya wanandoa kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake na kutoka nje kwenda kutafuta mtu wa kumridhisha zaidi, hata hivyo kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa huku anapata maumivu au kuumia kwa kuogopa kwamba asipompa Mume wake haki yake basi anaweza kutoka nje na kutokuwa mwaminifu hilo si sahihi kwani ni kutojiamini na kutojali si afya yako tu bali haki yako ya msingi ya kufanya tendo la ndoa kwa kupata raha.
Mnahitaji kujulishana na kuelezana ukweli ili muweze kupata dawa na hatimaye kurudi kwenye raha upya badala ya kuumizana.

Kuna mambo mengi yanayosababisha mwanamke au hata mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na inaweza kuwa ni wakati mwanaume anapoingia (penetrate) au wakati wa kitendo chenyewe au baada ya kitendo chenyewe.
Inaweza kuwa ni maumivu makali sana au inaweza kuwa ni kuwashwa au inaweza kuwa ni maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida au inaweza kuwa ni maumivu ambayo unasikia kama moto unawaka vile ndani yako wakati wa tendo la ndoa.


TIBA YA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA
 
EWE MWANAMKE FURAHIA NDOA YAKO KWA KUTUMIA SOY ISOFLAVONE.
Hiki ni kirutubisho kilichotengenezwa kwa maharage ya soya na njegere.Isoflavine ambayo ni mahususi kwa vichocheo vya kike Kama Estrogen.

Kazi kubwa ya Soy Isoflavone

1.Inasaidia mfumo wa uzazi kwa mwanamke,kufanya kazi vizuri na kuimarisha Mayai yake kupevuka.
2.Kuongeza Kazi za ovary Kama ulishawahi kutumia njia ya uzazi wa mpango na kwa sasa unahitaji mtoto.
3.Kutibu maumivu wakati wa tendo la ndoa.
4.Kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.
 5.Inaondoa matatizo ya maumivu ya mifupa,na matatizo yote yanatokea wakati wa kuingia Kwenye ukomo wa hedhi (menopause).
6.Inachelewesha kuzeeka mapema na kufanya ngozi kuwa na afya na ang'avu.

NOTE:Wanawake wengi wana upungufu wa Estrogen au kuongezeka kwa vichocheo kunakosababisha kupunguza kiasi cha damu kinachoenda Kwenye via vya uzazi na kusababisha kupungua kwa majimaji ukeni.Kama una matatizo hayo jipatie kirutubisho hiki.

KWA MAWASILIANO ZAIDI CALL/WHATSAPP
 +255 787218159
       +255 764218159.




Wednesday, 1 July 2015

 
Insomnia ni nini?
Huu ni ugonjwa ni ugonjwa ambao huambatana na tabia zifuatazo..
  •  Kushindwa kupata usingizi kabisa.
  • Kulala na usingizi kuisha usiku sana na kushindwa kulala tena.
  • Kubadilika kwa mfumo wa kulala mfano  mtu wa aina hii husinzia mchana na kukosa usingizi usiku.
  • Kusinzia haraka baada ya kufika kitandani  na usingizi kuisha haraka kisha kushindwa kupata usingizi tena.
Ugonjwa huu husababishwa na nini?
  •      Utumiaji wa madawa kama cocaine, nicotine,cafaine na unywaji wa pombe uliopitiliza.
  •     Magonjwa ya moyo ambayo humfanya mtu ashindwe kupumua vizuri wakati wa kulala.
  •   Maumivu makali ya mwili kama kidonda, kuvunjika mfupa, misuli na kadhalika.
  •  Matatizo ya mfumo wa chakula kama kiungulia na kupata choo ngumu.
  •     Mazingira mabaya ya kulala kama kelele nyingi na harufu kali.
  •  Msongo mzito wa mawazo
  • Utumiaji wa ovyo wa dawa za kuleta usingizi mfano diazepam maarufu kama valiam.
  • Upungufu au ongezeko la homoni za uzazi hasa kipindi cha uzeeni kwa wanawake{menopause} .
MATIBABU
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyka katika sehemu kuu mbili kama ifuatavyo.
Matibabu yasiyotumia dawa{non pharmacological treatment}:
kikubwa kinachofanyika hapa ni kuacha tabia zote ambazo ziko ndani ya uwezo wako ambazo zinakufanya ukose usingizi kama nilivyozianisha hapo juu. Aina hii ya matibabu ni nzuri na bora zaidi kuliko matumizi ya dawa za kuleta usingizi ambazo mara nyingi zinasababisha kuzitegemea yaani bila hizo haulali{dependence} na kuleta madhara mengine ya kiafya.
  •   Usile chakula kingi wakati wa kwenda kulala.
  • Usinywe kahawa wakati wa kwenda kulala
  • Kitanda kitumike kama sehemu ya kulala sio kuangalizia video na kucheza game.
  • Usiangalie video za kutisha wakati wa kwenda kulala.
Matibabu ya dawa
 
Magonjwa yanayosababisha{underlying causes} mtu kushindwa kulala yanatakiwa yatibiwe kwanza. mfano maumivu makali  ya mwili kutokana na magonjwa flani.
dawa ya kutibu tatizo la kutopata usingizi ni MELATONIN SOFTGEL CAPSULES
kuipata dawa wasiliana nami kwa simu no +255787218159

Monday, 22 June 2015













Kukosa choo kwa siku moja kitaalamu,  siyo tatizo, isipokuwa mtu anaweza kutajwa kuwa na tatizo hilo iwapo atakosa choo kwa angalau zaidi ya saa 72, yaani siku tatu.


kawaida kila mtu anatakiwa apate choo angalau mara tatu kwa wiki. “Kama mtu atakosa choo kwa siku tatu mfululizo, atahesabika kuwa na tatizo, lakini lazima awe amekula chakula kwa siku zote hizo.
Mtu ambaye hajala hawezi kuhesabika kuwa na ugonjwa huo bali atakuwa na tatizo jingine.

Zipo sababu nyingi  zinazosababisha tatizo la haja kubwa zikiwemo za kutojizoeza kwenda haja kubwa mara kwa mara, kula vyakula vilivyokobolewa,  matumizi mabaya ya dawa, mabadiliko ya homoni na magonjwa mengine ya mwili,kuwa na msongo wa mawazo pia kunaweza kupelekea mtu kutokupa choo.

MATATIZO YANAYOSABABISHWA NA KUKOSA CHOO.

Kukosa choo linaweza kuwa tatizo, lakini kama halitapatiwa ufumbuzi linaweza kuzaa matatizo mengine mwilini.



Dalili za kuwa na tatizo la kukosa ni kwamba mgonjwa anaweza kupata maumivu ya tumbo ambayo hutokana na tumbo kujaa gesi. Mtu mwenye tatizo la kukosa choo mara nyingi tumbo lake huvimba na kujaa gesi muda wote, hali hii inatokana na kuwa na uchafu tumboni.

Pia kukosa choo kunaweza pia kusababisha maambukizi katika utumbo ambayo yanaweza pia kusababisha magonjwa mengine ukiwamo wa kuoza kwa sehemu ya utumbo.
Kinyesi kinapokwama mahali, eneo lile linaweza kukandamizwa na kukosa damu, hivyo linaweza kuoza.

Ugonjwa mwingine unaoweza kuupata kwa kukosa choo ni  uvimbe katika njia ya haja kubwa (Bawasiri)  ambao nao husababishwa na kuchubuka mara kwa mara wakati wa kujisaidia.
Ngozi ya njia ya haja kubwa inapopata michubuko mara kwa mara, hupasuka na kusababisha vivimbe vidogo ambavyo huweza kukua kadri hali hiyo inayoendelea.


WAKINA NANI HUUGUA HUU UGONJWA.

Kwa kawaida tatizo hili huwapa watu mbalimbali duniani kote, lakini hutofautiana ukubwa wake kutokana na mifumo ya maisha, kwani wengine huwa wepesi kuligundua na kulitafutia ufumbuzi. Karibu kila mtu duniani katika  hatua fulani ya maisha hupata tatizo hili, kutokana na sababu za vyanzo vyake watu hupitiwa au kwa makusudi huacha kufuata kanuni na kujikuta wamepata tatizo hili.


Mfano wakati wa sherehe au mikusanyiko ya watu huwa ni vigumu kuchagua aina ya vyakula na wakati mwingine matunda na maji ya kutosha hukosekana hivyo kuwafanya watu wale vyakula  vigumu ambavyo vinaweza kuchochea tatizo hili.


Dawa ya kutibu tatizo la kukosa choo
Kinga na matibabu yake
Kila mtu anao uwezo wa kujikinga na tatizo hili kwa kufuata kanuni za ulaji chakula bora.
Njia sahihi ya kujikinga na ugonjwa huo ni kula nafaka zisizokobolewa, matunda, mboga mboga na kunywa maji kwa wingi.
Kuhusu matibabu halisi iwapo tatizo litagundulika mapema ni rahisi kulikabili kwa kubadilisha mfumo wa ulaji akitolea mfano mtu anapokosa choo na kuamua kula mapapai kwa wingi .
Kama mgonjwa akishindwa kutumia tiba mbadala ambazo ni pamoja na kula matunda, mboga na kunywa maji mengi, anaweza kutibiwa kwa kupewa dawa mbalimbali  kama ALOE ambazo zinaweza kumsaidia ili apate choo.
Hata hivyo, hilo linaposhindikana kwa njia zote hizo, mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuondoa kinyesi kile kilichoganda na kumwanzishia matibabu ya kumfanya aweze anajisaidia kwa urahisi.

wasiliana nami kujipatia dawa kabla tatizo halijawa kubwa.
+255 787 218159
+255 764 218159