Thursday, 28 May 2015


wanafunzi wakiwa tayari kwaajili ya maandamano ya siku ya hedhi
Siku ya hedhi duniani huazimishwa kila mwaka tarehe28/05 na kwa Tanzania kwa mwaka  huu ndio mara ya kwanza kushiriki kuazimisha siku ya hedhi duniani na kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni"HEDHI SALAMA TUWE PAMOJA".siku ya hedhi duniani ilianzishwa ili kuongelea swala zima la hedhi kuanzia ngazi ya familia ili kuondoa na kuvunja ukimya kwa wazazi na pia katika mashule walimu wanatakia kuwatambua mabinti wanapokuwa katika hedhi kwani wanakutana na changamoto nyingi kama vile kuumwa kichwa,kuumwa tumbo,kuumwa kiuno na wengine hata kutapika. na vile vile je nyumbani au mashuleni kuna mazingira salama yanayomruhusu binti kujiweka safi na kupata vifaa muhimu anavyohitaji kuvitumia akiwa katika hedhi mfano pedi,maji,na faragha na je vifaa vya kujisitiri vinapatikana? na je anajua jinsi ya kuvitumia? na je vifaa ni salama? na je kama shuleni hakuna mazingira rafiki kwa huyo binti ni sahihi kwa huyo binti kupoteza amsomo? na je hivyo vifaa vya kutumia wakati wa hedhi vinapatikana maeneo yote wanapopatika mabinti hasa vijijini? na kama binti analelewa na baba peke yake je anapata bajeti ya kununua vifaa vya kujisitiri wakati wa hedhi. mabinti wengi wamekuwa wakipitia changamoto nyingi wakati wa hedhi ambapo changamoto hizo zimepelekea mabinti hao kuacha shule na kushindwa kufikia malengo yao katika maisha na vile vile kupunguza mahudhurio hafifu mwiongoni mwa wanafunzi wa kike.Na hizo changamoto wanazozipitia mabinti ndizo zilizopelekea kuanzishwa kwa siku ya hedhi duniani ili kujenga  uelewa katika ngazi zote kwamba swala la hedhi kwa mabinti ni jukumu letu sote na sio la mabinti na wazazi wa kike pekee yao na pia kuhamasisha mabadiliko ndani ya jamii hususani mila na desturi zinazosababisha suala la hedhi kwa mwanamke lionekane kma ni jambo la aibu katika jamii zetu.

0 comments:

Post a Comment